Baraza Jipya La Taifa La Mashujaa Laapishwa
Jaji Mkuu Martha Koome amesema kuwa kuna haja ya kuwatambua wapigania uhuru waliosalia kwa juhudi zao za kuikomboa nchi kutoka kwa utawala wa kikoloni.
Jaji Mkuu wakati uo huo amelitaka Baraza la Mashujaa la Kitaifa kuunda miundo ya kuwaenzi mashujaa kama vinara wa msukumo kwa vizazi vijavyo.
“Siku zote tukumbuke kwamba kupitia vitendo vyao vya ushujaa, uadilifu na ukakamavu, mashujaa wetu wametoa mchango mkubwa katika nyanja na nyanja mbalimbali zinazounda msingi wa taifa letu,” alisema.
“Baraza la Kitaifa la Mashujaa lazima lifanyie kazi kubuni njia na njia ambazo sisi kama taifa tunaweza kuheshimu ujasiri wao, kujitolea kwao na moyo wa kutokemea ambao umeunda utambulisho wa taifa letu tunalopenda, Kenya,” CJ Koome aliongeza.
Jajai Koome amezungumza hayo hii Jumanne wakati wa hafla ya kuapishwa kwa Dkt. Chris K. Kiptoo kama mwanachama wa Baraza la Kitaifa la Mashujaa, na Charles Onyango Wambia, kama Afisa Mkuu Mtendaji wa Baraza.
Baraza limeeleza dhamira yake katika kusukuma uundwaji upya kwa vikundi vya wapigania uhuru wote waliosalia.