Home » Shollei:Kenya Lazima Ipitishe Mswada Wa 2023 Ili Kuwa Na Uchumi Bora

Shollei:Kenya Lazima Ipitishe Mswada Wa 2023 Ili Kuwa Na Uchumi Bora

Naibu Spika wa Bunge la Kitaifa na Mwakilishi wa Wanawake wa Uasin Gishu Gladys Boss Shollei ametoa maoni kwamba kuna haja ya kuwa na hatua kali zilizowekwa na serikali ili kuwaondoa Wakenya kutokana na hali mbaya ya kiuchumi.

 

Amesema hayo alipokuwa akitetea mapendekezo yaliyotolewa katika Mswada wa Fedha wa 2023 ambayo tangu wakati huo yameibua mizozo kati ya viongozi walioketi katika Bunge la Kitaifa na Seneti.

 

Kulingana na Shollei, mswada huo umejikita katika kuwapunguzia kipato cha chini (hustlers) kutoka kwa mzigo wa ushuru uliopo kwa kusumbua uagizaji wa baadhi ya bidhaa ili kuhimiza uzalishaji wa ndani na hatimaye kupunguza ukosefu wa ajira.

 

Akiongea kwenye kipindi cha runinga hii leo Jumatatu, Shollei ameteta kuwa Wakenya wanadanganywa na wale wanaopinga mswada huo na badala yake wanapaswa kuchukua muda kuchunguza mapendekezo hayo.

 

Mbunge huyo wa kaunti ya Uasin Gishu ameongeza kuwa kutokana na nia ya wazi ya mapendekezo hayo, atapiga kura ya ndiyo punde tu mswada huo utakapowasilishwa bungeni mnamo Juni 15 kwa mjadala.

 

Ili Kenya itoke kwenye mteremko wa sasa uliopo, Shollei amesema kuna haja ya kuwa na hatua kali na zisizostarehesha kutekelezwa.

 

Akitoa mfano wa Singapore, ambako serikali itakuwa ikikopa mifano ili kufanikisha mradi wake wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu, Shollei amesema kuwa waliwahi kuwa katika hali mbaya kama ya Kenya na wasingeweza kupata mafanikio yake ya kimaendeleo kama si kwa mageuzi waliyoyafanya.

 

Huku hayo yakijiri muungano wa Azimio umeashiria kuanzisha tena maandamano dhidi ya serikali iwapo mswada tata wa 2023 hautapitiwa upya huku Naibu Rais Rigathi Gachagua akisisitiza kuwa mswada huo utapitishwa bungeni.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!