Home » Orengo Kwa Wabunge: Msiwaache Wakenya Wakati Wa Huu Shida

Orengo Kwa Wabunge: Msiwaache Wakenya Wakati Wa Huu Shida

Gavana wa Siaya James Orengo amewataka Wabunge kuzingatia malalamiko ya umma kuhusu masuala ya Mswada wa Fedha wa 2023.

 

Orengo amesema walipa ushuru tayari wameelemewa na kuidhinisha mapendekezo ya nyongeza ya ushuru ya Kenya Kwanza kutawalemea wananchi ambao tayari wanahisi kubana kwa mfumuko wa bei.

 

Orengo alipokuwa akizungumza wakati wa mazishi ya Patrick Obuong’ Wandare katika eneo bunge la Gem, aliwasihi wabunge hao kutosaliti umma wakati wa mjadala wa mswada huo uliopangwa kufanyika wiki ijayo, akiongeza kuwa walipa ushuru tayari wameelemewa na kuidhinisha mapendekezo ya Kenya Kwanza ya kuongeza ushuru kutawalemea.

 

Gavana huyo amewaonya wabunge dhidi ya kukerwa na propaganda kutoka kwa utawala wa Kenya Kwanza kwani zitaitumbukiza Nchi katika matatizo zaidi.

 

Ni lazima (wabunge) wasikilize ili tuwe nao katika Muswada wa Marekebisho. Tunapokuwa na marekebisho basi itawezekana kusaidia ukuaji wa uchumi,” alisema Orengo.

 

Muda wa kupitishwa kwa Mswada huo ni tarehe 30 Juni ambayo itaambatana na kupitishwa kwa Sheria ya Matumizi ya Fedha, 2023.

 

Mswada huo, ambao una vifungu 84, unalenga kurekebisha sheria mbalimbali za ushuru na sheria zinazohusiana ili kupanua wigo wa ushuru na kuruhusu Mamlaka ya Ushuru ya Kenya kupata mapato zaidi, haswa kutoka kwa maeneo ambayo kijadi hayajashiriki kikamilifu katika kuchangia kapu la ushuru nchini.

 

Orengo aliandamana na Spika wa Siaya George Okode alitetea bunge kuhusu azma yao ya kumtimua Naibu Gavana wa Siaya William Oduol.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!