Home » Gavana Wa Isiolo Abdi Guyo Aaga Uhuru Na Kujiunga Na Ruto

Gavana Wa Isiolo Abdi Guyo Aaga Uhuru Na Kujiunga Na Ruto

Gavana wa Isiolo, Abdi Ibrahim Guyo, na naibu wake James Lowasa wamegura chama cha Jubilee na kujiunga rasmi na United Democratic Alliance (UDA) hii leo Ijumaa, Juni 2.

 

Wawili hao walijumuika na spika wa bunge la Kaunti ya Isiolo Mohamed Koto na mwenyekiti wa Orange Democratic Movement (ODM) Hassan Galma.

 

Guyo, aliyekuwa Mwakilishi wadi wa Wadi ya Matopeni jijini Nairobi, alichaguliwa kuwa gavana wa Isiolo kwa tiketi ya Chama cha Jubilee chini ya muungano wa Azimio La Umoja.

 

Alikuwa mtu wa kwanza kupaa kutoka mwakilishi wadi hadi Gavana tangu kupitishwa kwa Katiba ya 2010.

 

Kuingia kwake kwa UDA kunakuja wiki mbili baada ya Rais William Ruto kuzuru Kaunti ya Isiolo kwa ibada ya madhehebu mbalimbali mnamo Mei 21. Hii ilikuwa ziara yake ya kwanza katika eneo hilo tangu achaguliwe mwaka jana.

 

 

 

Hatua hiyo ilionekana kama jaribio la Ruto kujumuisha uungwaji mkono katika eneo ambalo lilipiga kura dhidi yake katika uchaguzi wa Agosti 2022.

 

Kuingia rasmi kwa Guyo kwenye UDA kumesimamiwa na Katibu Mkuu wa UDA Cleophas Malala, aliyepewa jukumu la kuongeza wanachama wa chama hicho kote nchini.

 

Jubilee chini ya Azimio La Umoja imegawanyika, huku mrengo mmoja ukiongozwa na Rais msaafu Uhuru Kenyatta na mwingine Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Kanini Kega akishirikiana na Ruto.

 

Kiongozi wa chama cha Azimio, Raila Odinga, alitishia kuitisha maandamano akionya UDA na muungano wake wa Kenya Kwanza, dhidi ya kuingilia vyama tanzu vyake.

 

Kega, kabla ya kujiuzulu na kujiunga na Jubilee, alikuwa mmoja wa Azimio, na nyongeza ya Guyo huenda ikazidisha mzozo kati ya Ruto na Raila, haswa huku mazungumzo ya pande mbili yakiwa tayari yamesitishwa.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!