Koigi Wa Mwere Asema Matarajio Ya Kenya Hayajaafikiwa
Aliyekuwa mbunge wa subukia Koigi wa Wamwere anasema matarajio ya wa kenya baada ya kujitawala bado hajaafikiwa hadi kufikia sasa huku kenya ikiadhimisha miaka 60 ya kujitawala.
Kwa mujibu wa Koigi, ukosefu wa kazi makazi duni,ufisadi,ukabila pamoja na utawala mbaya miongoni na masua mengine nyeti yamesalia kero hata baada ya mkoloni kuondoka
Kwa upande wake mchanganuzi wa masuala ya kisiasa Dkt. Abdul Noor, serikali zote tano za hapa Kenya zina ahadi nyingi ilhali hakuna hata serikali moja ambyo imetimiza ahadi zake kwa wakenya huku akihoji ni bora kuwa na wakoloni kuliko mwafrika ambaye hana utu kwa wafrika wenzake
Noor aidha anasema vingozi wa Afrika wa historia ya kujinufaisha wao pamoja na familia zao bila kumuangazia mwananchi aliyewachagua.
Taifa hili linahitaji kiongozi ambaye atanyenyekea kama joshua ili tufike tufike canaan, si lazima awe tajiri, na wala si mfisadi, ndo kauli yake koigi akikunja jamvi katika mazungumzo hayo hii leo alhamisi asubuhi.
Hata hivyo, viongozi hao wawili kwa kauli moja wamemtaka mkenya, mpiga kura kuwa makini kwani shida za kenya zinatokana na maamuzi mbaya ya wananchi kuwachagua viongozi wasiofaa mara kwa mara.
Itakumbukwa kwamba Koigi alikuwepo wakati wa Mau Mau ambapo amepinga kauli za naibu rais Rigathi Gachagua kwamba yeye ni kutoka familia ya Mau Mau akidai viongozi wenyewe wanajuana.