Home » Washukiwa Wanane Wakamatwa Kuhusu Kupotea Kwa Mifuko 4,520 Ya Mbolea

Washukiwa Wanane Wakamatwa Kuhusu Kupotea Kwa Mifuko 4,520 Ya Mbolea

Washukiwa wakiwa Milimani law courts. Picha: DCI/Twitter

Watuhumiwa wanane walifikishwa mahakamani Jumatano wakihusishwa na upotevu wa mifuko 4,520 ya mbolea ya ruzuku ya serikali iliyokuwa ikitumwa katika maeneo mbalimbali mwezi uliopita.

 

Wale wanane; Joseph Muthama, Stanely Muthama, Martin Munyao, Joseph Muthama, Eric Ng’ang’a, Fredrick Gateri, Anthony Ngei na Beatrice Mwikali, walifikishwa mbele ya mahakama ya Milimani.

 

Kwa mujibu wa Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), watuhumiwa hao walishtakiwa kwa kula njama na kutenda kosa kinyume na kifungu cha 393 na kuiba bidhaa zinazosafirishwa kinyume na Kifungu cha 297(c) cha Kanuni ya Adhabu.

 

Aidha Walikana mashtaka dhidi yao.

 

Kulingana na DCI, wanane hao wanadaiwa kunasa lori 10 zilizopewa kandarasi na Kampuni ya Kitaifa ya Biashara ya Kenya (KNTC) mjini Mombasa kusafirisha tani 281 za mbolea hadi kaunti mbalimbali nchini kati ya Aprili 18 na 27 mwaka huu.

 

Meneja wa usafirishaji wa KNTC aliripoti kisa hicho baada ya malalamiko kuwasilishwa katika Kaunti ya Nandi ikionyesha kuwa magunia 560, ambayo yalitumwa Aprili 27, yakipelekwa kwa Bodi ya Kitaifa ya Nafaka na Mazao (NCPB) huko Lessos, Kaunti ya Nandi, yalikuwa hayajawasilishwa siku chache baadaye. .

 

Uchunguzi wa wapelelezi baadaye uligundua kwamba kati ya lori 10 zilizokuwa zikitoa mbolea hiyo, ni mawili pekee yaliweza kufika maeneo yalikoenda huku nyingine nane zilizokuwa zimebeba takriban mifuko 4,529 ilitoweka kimaajabu na haijapatikana.

 

Operesheni ya haraka ilipelekea kukamatwa kwa washukiwa wanane huku makachero wakiendelea kuwafuata washirika wao ambao wanaamini bado wanajificha.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!