Home » Familia Za Waathiriwa Mukumu Girls Kupokea Ksh.400k

Wazazi wa wanafunzi waliofariki baada ya kisa cha kula sumu katika Shule ya Upili ya Wasichana ya Mukumu watapokea Ksh.ELFU MIA 400, 000 kila mmoja kama fidia kutoka kwa serikali.

 

Haya ni kulingana na Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu ambaye ameambia Seneti kwamba serikali itatumia Ksh M 1.2 kuwafidia wazazi wa wanafunzi 3 walioangamia kutokana na sumu ya chakula shuleni.

Akijibu swali la Seneta wa Kakamega Bonny Khakwale, Machogu hata hivyo amesema baada ya uchunguzi, serikali haitafungua mashtaka yoyote ya jinai dhidi ya aliyekuwa mkuu wa shule hiyo Fridah Ndolo au wasimamizi wa shule.

 

Amewaambia Maseneta hao kwamba timu ya mashirika mengi iliyochunguza tukio hilo haikupata hatia yoyote kwa upande wa usimamizi wa shule hiyo.

 

Machogu amedai kuwa hadi sasa, hakuna ushahidi kwamba ni mwalimu mkuu ambaye alikuwa akisambaza chakula shuleni ili kuwawezesha kumpata na hatia.

 

Hadi kufikia jana wanafunzi elfu 1962 walikuwa wameripoti shuleni, 44 bado hawajaripoti huku 56 wakiomba kuhamishwa kutoka shuleni.
Mlipuko huo ulisababisha zaidi ya wanafunzi mia 124 waliolazwa katika hospitali kuu ya kaunti ya Kakamega katika kisa kinachoshukiwa kuwa kula vyakula vya sumu na maji chafu.

 

Awali Mkurugenzi Mkuu wa Afya Patrick Amoth alisema chakula kilichotumiwa na wanafunzi kilikuwa na kinyesi cha binadamu.
Kufuatia tukio hilo, Waziri aliteua Jane Mmbone kama mwalimu mkuu wa shule hiyo na kumhamisha Mkuu wa Shule ya Mukumu Girl Frida Ndolo.

 

Katika hatua nyingine Waziri huyo pia alivunja bodi ya usimamizi ya shule hiyo ambayo hadi sasa imesababisha vifo vya wanafunzi watatu na mwalimu mmoja Alifanya mabadiliko hayo alipozuru shule kutathmini hali ilivyokuwa.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!