Home » Mwanafunzi Wa Darasa La 6 Amchoma Kisu Mwalimu Garissa

Kamishna wa kaunti ya Garissa Boaz Cherutich amewaonya wanafunzi kutowashambulia walimu shuleni akisema watakaopatikana na hatia watakabiliwa na mkono wa sheria.

 

Aidha amewataka wazazi na walimu kushirikiana ili kupunguza matukio ya utovu wa nidhamu shuleni.

 

Maoni yake yalikuja baada ya mzozo na mwanafunzi wa darasa la 6 na kumwacha mwalimu wa shule na majeraha mabaya.

 

“Juzi tumekuwa na kisa Garissa town ambapo mwalimu mmoja mwanamke alikuwa darasani, alipigwa na mwanafunzi wa darasa la 6,” Boaz alisema.

 

“Si hiyo ni aibu kubwa sana? Na tulishika wazazi tukaweka ndani ili tueleze sheria lazima ifanye kazi,”

 

Kulingana na ripoti, mwanafunzi huyo alimvamia mwalimu wake baada ya kuulizwa kwa nini alikuwa bado hajahudhuria masomo tangu shule zifunguliwe.

 

Mwanafunzi huyo anadaiwa kuondoka shuleni hapo baada ya kuzozana na kurejea muda mfupi baadaye akiwa na kisu ambacho alikitumia kumchoma mwalimu huyo sikioni.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!