Home » Mudavadi Kumwakilisha Rais Ruto Nigeria

Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi jana Jumapili ameondoka nchini kuelekea kule Nigeria Abuja kumwakilisha Rais William Ruto katika sherehe za kuapishwa kwa rais mteule Bola Tinubu hii leo Jumatatu.

 

Kabla ya kuapishwa kwa Tinubu, Rais Ruto aliipongeza Nigeria, ambayo aliitaja kuwa mshirika mkubwa wa kibiashara, na rais wake mpya na kuwatakia kila la heri.

 

Aidha rais ruto alidai Serikali ya Kenya inaahidi kushirikiana kwa karibu na utawala unaokuja kwa umiliki wa mafanikio na wa amani kulingana na taarifa kutoka kwa mkurugenzi wa vyombo vya habari wa Mudavadi Salim Swaleh.

 

Tinubu mwenye umri wa miaka 71, ataapishwa kama rais wa kumi na sita wa Nigeria na anachukua nafasi kutoka kwa Muhammadu Buhari mwenye umri wa miaka 80 ambaye muhula wake a uongozi umekamilika.

 

Licha ya upinzani kudai kuwa kulikuwa na udanganyifu katika uchaguzi huo, maafisa wa uchaguzi wamesema upigaji kura ulikuwa huru na wa haki na hivyo kumtangaza Tinubu kuwa mshindi.

 

Yakijiri hayo… Rais wa zamani Uhuru Kenyatta amemtaka rais anayekuja wa Nigeria Asiwaju Bola Tinubu kujitahidi kuwa jambo la kuunganisha Wanigeria wote anapojitayarisha kuchukua madaraka.

 

Uhuru alizungumzia kuapishwa kwa rais wa Nigeria mjini Abuja ambapo pia alionya dhidi ya mitego ya kile alichokitaja kuwa masuala yanayokandamiza demokrasia barani afrika.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!