Home » Video Yanasa Ghorofa Likiporomoka Mombasa

Jengo katika eneo la Marikiti kaunti ya Mombasa limeporomoka hii leo Jumamosi, Mei 27 baada ya kupata nyufa kadhaa.

 

Taarifa zimeeleza kuwa wakazi kadhaa walijeruhiwa na kukimbizwa hospitalini huku shughuli za uokoaji zikiendelea katika tukio hilo lililotokea dakika chache baada ya saa 1:00 mchana.

 

Chanzo kilicho karibu na tukio hilo kiliithibitishia kwamba Gavana wa Mombasa Abdulswamad Sharrif Nassir alikuwa katika eneo la tukio pamoja na maafisa wengine wa dharura na maafisa wa polisi kutoa waliokwama kwa vifusi.

 

Kulingana na wakazi hao, nyumba hiyo ilikuwa imeonyesha dalili za kupomoka huku wapangaji watakiwa kuhama mara moja kutokana na hatari inayowakabili.

 

Aidha visa vya majengo kuporomoka vimeendelea kugonga vichwa vya habari kote nchini haswaa baada ya ghorofa kadhaa kuporomoka na kuwauwa watu kadhaa sehemu za Nairobi na Kiambu huku wengine wakiachwa na majereha mabaya zaidi.

 

Kwa sasa wakenya wameomba serikali kuingilia kati na kuwamata maafisa waohusika katika ufisadi wa kuitisha hongo na kuacha majengo kama kujengwa bila kuidhinishwa na vitengo husika.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!