Home » Serikali Yaonya Wakenya Dhidi Ya Bidhaa Ambazo Hazijaidhinishwa

Serikali Yaonya Wakenya Dhidi Ya Bidhaa Ambazo Hazijaidhinishwa

Shirika la Viwango nchini (KEBS) leo hii Ijumaa, Mei 26, limewaonya Wakenya kuhusu bidhaa zisizo na alama za udhibitisho la shirika hilo.

 

Katika notisi, wakala wa serikali wamebaini kuwa baadhi ya wafanyabiashara walikuwa wakikiuka sheria za soko kwa kuingiza bidhaa za sokoni ambazo hazijaidhinishwa na KEBS.

 

Waagizaji, watengenezaji, wauzaji reja reja, wenye hisa na wafanyabiashara wengine wamekuwa miongoni mwa wafanyabiashara walioonywa kwa kukiuka viwango vya bidhaa hizo kulingana ana katiba Sura ya 496.

 

Kufuatia kuenea kwa bidhaa ambazo hazijaidhinishwa sokoni, KEBS imefafanua kuwa haitawajibikia bidhaa zozote zitakazonunuliwa bila viwango Hivyo kuwashauri Wakenya kuangalia uhalisi wa bidhaa yoyote kabla ya kununua.

 

Ili kukabiliana na ongezeko la bidhaa ambazo hazijaidhinishwa, KEBS sasa imezindua msako wa kitaifa Katika operesheni hiyo, shirika hilo limesisitiza kuwa bidhaa zozote ambazo hazijaidhinishwa zitakamatwa na kuharibiwa papo hapo.

 

Hatua zaidi za kisheria pia zitawapata wafanyabiashara watakaopatikana na hatia.

 

Alama za KEBS ni muhimu kwa wanunuzi wote kwani inaonyesha mpango wa uidhinishaji wa bidhaa zinazotengenezwa nchini.

 

Kulingana na KEBS, bidhaa zinazozalishwa nchini zilizo na alama hiyo zinakidhi mahitaji ya ubora nchini.

 

Katika notisi hiyo, KEBS imefahamisha wafanyabiashara kwamba alama ya kusawazisha bidhaa hutolewa baada ya ukaguzi wa kiwanda na majaribio ya sampuli.

 

Mtengenezaji aliyeidhinishwa anahitajika kuzingatia mpango wa udhibitisho wa usimamizi katika muda wote wa uhalali wa miaka miwili.

 

KEBS pia hufanya ufuatiliaji na majaribio ya bidhaa zinazouzwa sokoni ili kuhakikisha kuwa watengenezaji wanatii baada ya kupewa kibali.

 

Alama zingine za ubora zinazochapishwa kwenye bidhaa ni pamoja na Alama ya Almasi ya Ubora, Alama ya Kuimarishwa kwa Ubora na Alama ya Kuweka Viwango vya Ubora.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!