Home » Kindiki: Baadhi Ya Waathiriwa Shakahola Walitoka Mataifa Mengine

Kindiki: Baadhi Ya Waathiriwa Shakahola Walitoka Mataifa Mengine

Baadhi ya waathiriwa wa “mauaji ya Shakahola” walikuwa raia wa wageni kutoka nchi jirani ndio kauli yake Waziri wa Mambo ya Ndani Kithure Kindiki .

 

Akifika mbele ya Kamati ya Muda ya Mashirika ya Kidini hii leo Ijumaa, waziri amesema uchunguzi wa awali unaonyesha baadhi ya waathiriwa walisafiri kutoka nchi jirani.

 

Kindiki hakuchelewa kusema kwamba wenyeji walikwepa kanisa la Mchungaji Paul Mackenzie baada ya kujifunza kuhusu njia zake potovu.

 

Waziri huyo alisema wengi wa waathiriwa wake walikuwa kutoka magharibi, Kaskazini mwa Kenya, Mashariki, Nyanza na baadhi ya maeneo ya Pwani.

 

Takriban miili 241 hadi sasa imefukuliwa kutoka kwa makaburi ya kina kifupi msituni tangu matukio ya kutisha ya ibada yalipojitokeza mnamo Aprili 14.

 

Uchunguzi wa miili 112 ya kwanza ulionyesha kuwa wengi wa wahasiriwa walikufa kwa njaa.

 

Baadhi ya waathiriwa, wakiwemo watoto, walinyongwa, kupigwa, mkuu wa oparesheni za uchunguzi, Johansen Oduor, alisema wiki mbili zilizopita.

 

Polisi hadi sasa wamewakamata watu 39 na kuwaokoa wengine 91 kutoka msituni.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!