Home » Octopizzo Awapiku Wasanii Wote Nchini

Rapa Henry Ohanga almaarufu Octopizzo amekuwa msanii wa kwanza kutoka Kenya kufikisha views milioni 1 ndani ya saa 36.

Octo aliachia wimbo mpya unaoitwa ‘Sijawai’ na wimbo huo umekusanya VIEWS zaidi ya milioni 1 ndani ya saa chache baada ya kupakiwa kwenye YouTube.

 

Video ambayo ilitolewa Mei 24, 2023, tayari inavuma katika nambari 27 kwenye YouTube.

 

Wimbo wa “WOMAN “wa Otile Brown na Harmonize ulikuwa ukishikilia rekodi hiyo baada ya kufikisha views milioni moja ndani ya saa 48.

 

Wimbo mwingine “Suzanna” wa Sauti Sol naye ilitazamwa mara 1M ndani ya siku tatu pekee, sawa na ‘Hatutaachana’ ya Diana B.

 

Kwa ujumla, Diamond Platnumz wa Tanzania na Rayvanny wanashikilia rekodi ya wasanii waliofanikiwa kufikisha views milioni moja ndani ya kipindi kifupi zaidi.

 

Mnamo Septemba 2019, Rayvanny aliyesainiwa na WCB aliweka rekodi mpya katika Tasnia ya Muziki barani Afrika, baada ya video yake inayoitwa “PEPETA” iliyomshirikisha mwigizaji na mwimbaji wa Bollywood Nora Fatehi kutazamwa mara milioni 1 ndani ya saa 6.

 

Video fupi ya sekunde 21 ilimsaidia VANNY Boy kusajili hatua mpya katika taaluma yake ya muziki.

 

Mnamo Novemba 30, 2020, Rais wa WCB Diamond Platinumz na Rhumba Maestro Koffi Olomide waliandikisha historia baada ya video ya #Waah kutazamwa zaidi ya watu milioni 1 ndani ya saa 8 na kutapata Views milioni 2 ndani ya saa 13 kwenye YouTube. Hadi sasa Waah ina views zaidi ya Milioni 78 na kadhaa.

 

Hii ilikuwa hatua mpya kufikiwa na msanii wa Kiafrika kwa kuzingatia ukweli kwamba video ya “Waah” iliweza kupata zaidi ya views milioni 2 kwa chini ya saa 24.

 

Video ya Waah imeongozwa na Director Kenny na mpaka sasa ina zaidi ya views milioni 136.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!