Wanafunzi 20 Wapoteza Fahamu Baada Ya Vitoza Machozi Kurushwa Shuleni
Wanafunzi 20 wamepoteza fahamu baada ya maafisa wa polisi wa kukabiliana na ghasia kuvamia kwa kutumia vitoa machozi katika shule yao iliyoko Kawangare Estate jijini Nairobi.
Imeripotiwa kuwa wanafunzi hao walikuwa wakisoma masomo ya asubuhi wakati maafisa wa polisi walipokabiliana na wafanyabiashara wa Kawangware kwa kuzua vurugu eneo hilo.
Wakati polisi wakifyatua vitoa machozi kuwatawanya wafanyabiashara hao, baadhi ya viliuzi hivyo vilitua katika shule ya jirani na kusababisha taharuki na kuwalazimu wanafunzi kutoroka ili kujilinda.
Hata hivyo, wanafunzi kadhaa hawakubahatika kwani waliathiriwa na moshi mwingi wa vitoa machozi uliokuwa ukifuka kwenye shule hiyo.
Wanafunzi walioathirika baadaye walipelekwa katika hospitali mbalimbali karibu na Kawangware Estate ambako walipata matibabu baada ya kubainika kupata matatizo ya kupumua.
Ilibainika kuwa wanafunzi waliosalia shuleni walikuwa katika hali shwari na hawakuhitaji huduma za hospitalini moja kwa moja.
Huku hayo yakijiri, maandamano hayo yalisababisha kutatiza kwa usafiri katika barabara ya Naivasha, Nairobi, baada ya wafanyabiashara waliokuwa na gadhabu kuwahusisha maafisa wa polisi katika vuta nikuvute.
Maandamano hayo pia yaliathiri barabara zilizo karibu zikiwemo zile zinazoelekea Riruta, Wanye na maeneo mengine ya Kaunti ya Kiambu.
Wafanyabiashara hao waliripotiwa kupinga uamuzi wa utawala wa Kaunti ya Nairobi kubomoa vibanda vyao vinavyodaiwa kujengwa kwenye njia na barabara kuu.
Polisi walikuwa na wakati mgumu kusafisha barabara ambazo waandamanaji walikuwa wamechoma matairi na kubomoa mabango ya kampeni ya Rais William Ruto.
Kulingana na Kifungu cha 37 cha Katiba, haki ya kukusanyika inaweza kuwekewa vikwazo katika hali fulani, kama vile wakati maandamano yana uwezekano wa kusababisha vurugu au kuvuruga utulivu wa umma.
Sheria ya Utaratibu wa Umma (2012) inadhibiti haki ya kukusanyika nchini Kenya. Sheria inataka kwamba mtu yeyote anayepanga mkutano wa hadhara au maandamano lazima aarifu polisi angalau siku tatu kabla.