Home » Bonfire Adventures Yamzawidi ‘Genius Boy’ Likizo Ya Mombasa

Bonfire Adventures Yamzawidi ‘Genius Boy’ Likizo Ya Mombasa

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Bonfire adventures Simon Kabu amemzawadia mtoto wa miaka mitatu mwenye ana uwezo wa kutaja majina ya Magavana na Wabunge kwa kumpeleka likizo hadi Mombasa.

 

Ethan wa Mercy Muthoni alipokuwa akijitambulisha alisambaa mitandaoni baada ya video yake akiwataja wanasiasa wa Kenya kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

 

Mtoto huyo wa miaka mitatu aliwashangaza Wakenya kwa uwezo wake wa kuwataja viongozi nchini pamoja na manaibu wao.

 

Simon Kabu alifurahishwa na mvulana huyo ambaye ndoto yake ni kwenda chuo kikuu cha Harvard na kuahidi kuwapeleka Ethan na mamake Mercy Muthoni hadi Mombasa kwa likizo ili pia apate uzoefu wa safari ya ndege katika shughuli hiyo.

 

Kabu pia ameahidi kujitokeza na kusaidia karo za shule na pia kumtafutia mama yake kazi. Pia alimuomba ampeleke mtoto Ethan bungeni ili aweze kuwaona viongozi hao ana kwa ana.

 

“𝐁𝐚𝐛𝐲 𝐄𝐭𝐡𝐚𝐧, 𝟑 𝐘𝐞𝐚𝐫𝐬 𝐎𝐥𝐝, 𝐈𝐬 a genius Na @bonfireadventures ina Furaha Kumtunuku Yeye na Mama Likizo Hii ya Mombasa.Tunaamini Katika Kusaidia na ku-support talanta mbalimbali.Pia tutamletea karo yake ya shule tunapojaribu kupatia mama kazi. Kwa wale wanaotaka kumfikia mama 𝐌𝐞𝐫𝐜𝐲 𝐨𝐧 𝟎𝟕𝟐𝟒𝟗𝟕𝟖𝟔𝟐𝟎 #bonfirerewardingheroes.”

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!