Home » Polisi Waanzisha Uchunguzi Baada Ya Catherine Njeri Kuanguka Hadi Kufa

Polisi Waanzisha Uchunguzi Baada Ya Catherine Njeri Kuanguka Hadi Kufa

Polisi wanachunguza kisa ambapo mwanamke mmoja alifariki baada ya kuanguka kutoka orofa ya nane ya jengo moja katika kijiji cha Gacharage, Kaunti ya Kiambu.

 

Maafisa wa upelelezi wamedai kuwa watu watano walikuwa na marehemu mwanamke aliyetambulika kama Catherine Njeri, wakati wa kisa hicho cha kusikitisha.

 

Aidha Njeri alikuwa mwanafunzi katika Taasisi ya Usimamizi ya Kenya.

 

Wakati wa tukio hilo alikuwa amemtembelea rafiki yake kwa karamu katika nyumba yao Jumapili iliyopita kabla ya msiba kutokea alipokuwa katika nyumba hiyo na mpenzi wa rafiki yake.

 

Washukiwa hao kwa sasa wanazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Karuri huku wapelelezi wakiendelea na uchunguzi kubaini chanzo rasmi.

 

Awali Washukiwa ambao ni marafiki zake walifikishwa mahakamani na polisi waliruhusiwa kuwazuilia kwa siku kumi wakisubiri uchunguzi.

 

“Polisi wameanzisha uchunguzi kuhusu hali ya kifo cha Catherine Njeri Washukiwa watatoa taarifa na kushirikiana kikamilifu na wapelelezi wetu ili kusaidia kufichua ukweli,” Naibu Kamishna wa Kaunti ya Kiambaa Peter Maina aliambia wanahabari Jumanne.

 

Wapangaji wa jengo hilo walisimulia wakati waliposikia kishindo kikubwa kilichovuta hisia zao.

 

Mwili wa marehemu umepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Kihara Level 4, ambapo uchunguzi wa kina utafanywa.

 

Walioshuhudia walisema kuwa marehemu alikuwa amewatembelea marafiki zake na walikuwa wanane kati yao katika nyumba hiyo.

 

Mwendo wa saa 9:30 usiku, Njeri aliondoka nyumbani akiwa na mpenzi wa rafiki yake na kwenda seheu iliyo juu ya paa ambapo walisimama.

 

Kulingana nao Inaonekana alikuwa ameenda kwenye balcony na mwanamume na mapambano yakatokea akiwa huko kabla ya kuanguka chini ambapo Wapangaji wengine walikimbia kuwaamsha waliokuwepo ambao hawakujua kwamba msichana huyo alianguka na kufa.

 

Haijabainika ni nini kilifanyika alipokuwa kwenye balcony na kumpelekea kuanguka.

 

Hili ni tukio la hivi karibuni zaidi kutokea katika siku za hivi karibuni eneo hilo.

 

Mnamo Februari 2023, mwanamke mwenye umri wa miaka 29, aliyejulikana kama Brenda Kawira Gitonga, alianguka hadi kufa kutoka ghorofa ya nne ya nyumba yake huko Kasarani.

 

Tukio hilo lilitokea baada ya mwanamke huyo kugombana na mpenzi wake ambaye alitoa maelezo ya kustaajabisha ya matukio ya siku hiyo.
Kulingana na mpenzi huyo, marehemu alivamia chumba ghafla na kwenda kwenye balcony.

 

Baadaye anasema, aligundua kuwa mpenzi wake alikuwa amekufa.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!