Home » Kenya Yafanya Mageuzi Katika Sekta Ya Afya

Katika harakati za kuleta mabadiliko katika utoaji wa huduma za afya na kukuza uwezo wa kujitegemea, kamati ya Wizara ya Afya ya Kenya ikiongozwa na Dkt. Patrick Amoth pamoja na Dkt. James Nyikal kutoka Kamati ya Bunge ya Afya, akiungana na Waziri wa Afya Nakhumicha S. Wafula wamekutana na Mkurugenzi Mtendaji shirika la GAVI Seth Berkley.

 

Kenya imekuwa ikiwekeza kikamilifu na kutekeleza mageuzi yanayolenga kubadilisha utoaji wa huduma za afya kote nchini.

 

Mojawapo ya vipaumbele muhimu kwa nchi katika kipindi cha miaka mitano ijayo ni Huduma ya Afya kwa Wote (U.H.C), huku chanjo ikipewa mstari wa mbele kutekelezwa.

 

Aidha Zaidi ya watoto wachanga milioni 1.5, wanawake wajawazito na wasichana elfu mia 700,000 hupokea huduma za chanjo ya bure kila mwaka.

 

Ikiwa na vituo 9,000 na zaidi vya afya, vikiwemo mashirika ya umma, ya kibinafsi, ya kidini na yasiyo ya kiserikali, Kenya imejitolea kulinda afya ya wakazi wake.

 

Wakati wa mkutano huo, muungano wa GAVI umeelezea nia yake ya kutoa msaada wa kifedha kwa Kenya kupitia Hazina ya kitaifa na pia kupanga ziara ya hali ya juu ili kuimarisha zaidi ushirikiano huo.

 

Kwa kutambua hitaji la kujitegemea na suluhu za kiubunifu, Wizara ya Afya, kupitia taasisi kama vile Kenya Biovax (K.B.I) na Taasisi ya Utafiti wa Matibabu KEMRI, huangazia utengenezaji wa chanjo na H.P.T.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!