Home » Museveni Atoa Makataa Ya Kuwafukuza Wakenya Uganda

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameomba serikali ya Kenya kufuata matakwa yake la sivyo wakenya wa jamii ya Turkana wanaoishi nchini mwake watafukuzwa ndani ya miezi sita ijayo.

 

Katika Agizo la Utendaji nambari 3 la 2023 la kurasa 18 lililoonekana na wanahabari, Museveni ameelezea kufadhaika kwake kwamba upole wake wa kuruhusu jamii ya Waturkana kulisha mifugo zao Uganda ulikabiliwa na uhasama kwani alidai walipeleka bunduki nchini Uganda.

 

Ameongeza kuwa hii ilisababisha kuongezeka kwa visa vya uhalifu katika eneo la Karimonjong ikiwa ni pamoja na wizi wa ng’ombe 2,245 kutoka kwa wakaazi wa Uganda.

 

“Hapo zamani za kale, niliwaamuru hawa Waturkana wasiwahi kuleta bunduki nchini Uganda. Wanapaswa kuja tu kuchunga ng’ombe wao isipokuwa wakiwa na silaha.

 

“Hata hivyo hawakusikiliza, badala yake walivamia Karimonjong wetu waliyonyang’anywa silaha, wakaua watu, kuwabaka n.k. Inasemekana walivamia ng’ombe 2245 kutoka kwa Jie. Waliwaua wetu 3 (watatu), mwanajiolojia, 1. Afisa na askari, waliokuwa wakiwalinda. Sasa naelekeza kwamba upuuzi huu wa Waturkana lazima ukome,” alisema.

Akigusia haya, Museveni ameitaka serikali ya Rais William Ruto kuwakabili wafugaji wa Turkana wanaotuhumiwa kuwaua wanajiolojia wa Uganda kwa kesi ya mauaji.

 

Amebainisha kuwa bunduki hizo zilirejeshwa kwa serikali ya Uganda, lakini sio wauaji waliotenda visa vya mauaji. Wakishafikishwa, wauaji wanapaswa kufanya tambiko la kimila kwa familia zilizofiwa ambapo wanatakiwa kutoa ng’ombe sawa na kile ambacho marehemu angechangia katika maisha yake.

 

Katika kesi kuhusu wizi wa ng’ombe 2,245, rais wa Uganda amebainisha kuwa Turkana inapaswa kutoa idadi sawa ya ng’ombe walioibiwa.

 

“Kupitia uratibu wa Serikali za Kenya na Uganda, Waturkana lazima warudishe kwa jamii zilizoathiriwa idadi ya ng’ombe sawa na ng’ombe walioiba kutoka kwao.

 

Zaidi ya hayo, ameonya kuwa Waturkana wanaovuka mpaka wakiwa na bunduki wana hatari ya kukamatwa na kushtakiwa kwa ugaidi na Mahakama ya Kivita.

 

Rais wa Uganda ameupa utawala wa Ruto muda wa miezi sita kufuata maagizo hayo, la sivyo atawatimua Waturkana wote wa Kenya na ng’ombe wao.

 

Hata hivyo, Waturkana wamepigwa marufuku kuingia tena Uganda na wanyama wao.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!