Home » Mwanafunzi Wa Kapsabet Boys Ajishindia Ksh3.5M

Shule ya Upili ya Wavulana ya Kapsabet katika Kaunti ya Nandi iliandaa shindano la hisabati mnamo Jumamosi, Mei 20 ambalo lilikuwa wazi kwa wanafunzi wa kidato cha 1 hadi cha 4 kutoka kote nchini.

 

Wakaguzi na wasimamizi walimazi kuhakiki alama kwenye mitihani na wakafikia mwafaka kwamba mwanafunzi wa kidato cha 4, Kelvin Kemboi, kutoka Shule ya Upili ya Kapsabet alikuwa ameshinda shindano hilo.

 

Kemboi alituzwa Ksh3.5 milioni katika ufadhili wa masomo, na atakuwa na fursa ya kusoma katika shule yoyote atakayochagua nchini Australia.

 

Akiongea na kituo moja cha habari nchini mwalimu wa Kemboi Oliver Toroitich alizungumza kwa fahari, akibainisha kuwa huenda mwanafunzi wake ataiongoza taifa katika mtihani wa kidato cha nne (KCSE) 2023.

 

Shindano hilo lilivutia zaidi ya wanafunzi 4,000 kutoka shule za upili za Kenya. Kusudi kuu la shindano hilo lilikuwa kuunda njia kwa wanafunzi kuonyesha ujuzi wao na kuongeza imani yao katika somo la hisabati.

 

Mashindano hayo yaligawanywa katika makundi mawili, ambayo yalikuwa ya mtu binafsi na timu yake Katika kategoria ya mtu binafsi, wanafunzi walipewa maswali ya hisabati kuyafanya kwa muda mfupi zaidi.

 

Wanafunzi watatu bora katika kila kategoria walitunukiwa zawadi Katika kategoria ya timu, wanafunzi waligawanywa katika timu za watu wanne na kupewa maswali kutatua pamoja.

 

Timu tatu za juu katika kila kategoria zilitunukiwa zawadi.

 

Mshindi wa jumla wa kitengo cha mtu binafsi alikuwa Kemboi kutoka Shule mwenyeji na alitunukiwa ufadhili wa kusoma nchini Australia katika chuo kikuu alichochagua.

 

Washindi katika vipengele vingine walitunukiwa karo ya mwaka mzima ya shule kwa mwanafunzi bora katika kila darasa.

 

Zawadi nyingine ni pamoja na vikombe kwa shule bora ya wavulana, shule bora ya wasichana, shule ya bweni iliyo na mchanganyiko bora na shule bora kwa ujumla.

 

Mshindi wa jumla wa kitengo cha timu alikuwa Timu A kutoka Shule ya Upili ya Wavulana ya Kapsabet waliotunukiwa zawadi ya pesa taslimu.

Tukio hilo liliadhimisha toleo la 20 la shindano la kila mwaka la hisabati, na lilifadhiliwa na Grace International Migration.

 

Idara ya Hisabati ya Shule ya Upili ya Kapsabet iliongozwa na Oliver Toroitich, mwalimu mwenye uzoefu ambaye aliwahimiza wanafunzi kubadilishana mawazo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!