Home » Huduma Za M-Pesa Hazitapatikana Leo

Picha kwa hisani

Kampuni ya mawasiliano ya Safaricom imetangaza urekebishaji wa mfumo uliopangwa ambao utaanza saa 11 usiku leo hii Jumamosi, Mei 20, hadi kesho saa 4 asubuhi Jumapili, Mei 21, 2023.

Kampuni hiyo, katika taarifa yake kwa umma iliyotolewa, imesema kuwa huduma kadhaa hazitapatikana katika muda uliowekwa, miongoni mwao ni malipo ya Bili na Kununua Bidhaa Lipa Na M-Pesa.

 

Huduma za Uhawilishaji Pesa za Kimataifa (Western Union) na M-Pesa Global, pamoja na Programu ya M-Pesa na Programu ya Safaricom pia zitazimwa.

 

Zaidi ya hayo, M-Shwari, KCB M-Pesa, M-Kesho, Hustler Fund, Fuliza New Limit, Pinless Up-up, na huduma za loT zitaathiriwa wakati wa marekebisho hayo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!