Home » Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta Amwomboleza Popsy Getonga

Rais wa zamani Uhuru Kenyatta na aliyekuwa Mkewe Rais Margaret Kenyatta wamejumuika na familia na marafiki kwa ajili ya misa ya marehemu Popsy Bastiana D’Souza Getonga, mke wa msaidizi wa kibinafsi wa Rais Mwai Kibaki Alfred Gitonga, katika Kanisa Katoliki la St. Austin’s Nairobi.

 

Hadi kifo chake, D’Souza alikuwa Balozi wa Utalii wa Ushelisheli na mhudumu wa utalii Nairobi ambaye ujuzi wake wa kibiashara ulipendwa sana katika sekta ya utalii.

 

D’Souza, almaarufu Popsy, alisifiwa na kusherehekewa na familia yake na marafiki kama mtu mchangamfu na mwenye shauku ambaye alipumua nguvu katika mazingira yake.

 

Rais huyo wa zamani, ambaye alikumbuka urafiki wao miaka ya nyuma huko Amherst College, Massachusetts, pamoja na mumewe Alfred na wenzao, wamemsifu Popsy kama rafiki mwaminifu ambaye hakuwahi kuogopa kusema mawazo yake.

 

Mkuu huyo wa nchi mstaafu amemtaja marehemu kuwa mtu aliyegusa maisha ya wengi kwa njia tofauti.

 

Viongozi wengine waliotoa heshima zao za dhati ni pamoja na Rais wa Ushelisheli Wavel Ramakalawan, ambaye rambirambi zake zilisomwa na mwakilishi wa serikali na kumpa pole marehemu kwamba alitekeleza majukumu yake kwa bidii.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!