Home » Ruto: Hata Marafiki Zangu Hawatahepa Shoka La Kukabiliana Na Ufisadi

Ruto: Hata Marafiki Zangu Hawatahepa Shoka La Kukabiliana Na Ufisadi

Rais William Ruto amesema hatakuwa na yeyote atakayekwepa katika kukabiliana na ufisadi nchini.

 

Rais ruto anasema hakuna atakayeponea shoka la mahakama hata marafiki zake akiongeza kuwa lazima Wakenya wapate thamani kwa kila ushuru wanaolipa.

 

Rais amesema hayo huko Kandara, Kaunti ya Murang’a, leo hii Ijumaa wakati wa mazishi ya David Wawerū Ng’ethe – babake Mbunge wa Dagoretti Kusini John Kiarie na kumtaja mbunge huyo wa zamani wa Kandara kuwa ni kiongozi aliyeheshimika, mwenye mawazo , mwelekeo dhabiti na mwenye malengo.

 

Rais ruto kwa mara nyingine amehakikishia nchi kuwa uchumi utarejea sawa hivi karibuni na kusisitiza kuwa hakuna sehemu yoyote ya Kenya itakayosalia nyuma kimaendeleo.

 

Waliohudhuria ni Mawaziri Njuguna Ndung’u, Alice Wahome Moses Kuria, Gavana Irungu Kang’ata, wabunge pamoja na wawakilishi wadi
Aidha Viongozi hao wamemtaka Rais Ruto kusalia imara katika vita vyake dhidi ya ufisadi huku Gavana Kang’ata akisema ni makosa kwa watu binafsi kufaidika na rasilimali za umma.

 

Haya yameungwa mkono na Mbunge wa Kikuyu Kimani Ichungw’ah aliyeshikilia kuwa Rais ni mtu dhabiti katika kulinda rasilimali za umma.

 

Kwa upande wake Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro alimuomba Rais kuongeza na kupanua hatua zake dhidi ya ufisadi.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!