Home » Wafanyabiashara Kariakoo Warejea Madukani

 

Wafanyabiashara wa soko la Kariakoo wamerejea madukani kwao na kuamua kufanya biashara baada ya mkutano wao na waziri Mkuu Kassim Majaliwa kufanyika siku ya  Jumatano katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.

 

SOMA PIA: Wafanyabiashara Kariakoo Waendeleza Mgomo

 

Katika wa mkutano huo, wafanyabiashara hao walielekeza kero zao na kero kubwa ikiwa ni gharama wanazotozwa katika kodi zinazopelekea wao kushindwa kufanya kazi zao kwa faida na kupelekea kufunga maduka tangu ilipotimu siku ya Jumatatu.

 

 

Mkutano huo uliomsimamisha Waziri mkuu kwa takribani masaa sita ulihitimika mara baada ya kuundwa kwa kamati ambayo itafuatilia masuala hayo ya ushuru pamoja na kodi wanazotozwa wafanyabiashara hao.

 

Mbali na hilo, pia uundaji wa kamati hiyo ulijumuisha wafanyabiashara wa soko  hilo pamoja na viongozi wa serikali ambao wote watafuatilia katika kero zinazowasibu wafanyabiashara hao ikiwemo changamoto kubwa ya kodi.

 

Soko la Kariakoo ni moja kati ya masoko makubwa katika biashara na limekuwa likitumika pia na wafanyabiashara wa nchi mbalimbali kama vile Malawi, Zambia, Kongo na nchi nyingine nyingi zinzoizunguka Tanzania.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!