Home » Mwalimu Kajiado Ashtakiwa Kwa Kujihusisha Na Ushoga

Mwalimu mmoja wa Shule ya Sekondari amekamatwa na kufikishwa katika Mahakama ya Sheria ya Kajiado kwa madai ya kulawiti mpwa wake wa miaka 16.

 

Mtuhumiwa George Sane mwenye umri wa miaka 30, amewasilishwa mbele ya Hakimu Mkuu Edgar Kagoni akishtakiwa kwa kumlawiti mwanafunzi huyo kwa tarehe tofauti kati ya Desemba mwaka jana na Aprili mwaka huu wakati mvulana huyo alipopashwa tohara na kuwekwa chini ya uangalizi wake madaia ambayo mshtakiwa amekana na kuachiliwa kwa bondi ya Ksh.elfu mia 400,000.

 

Aidha Mshtakiwa huyo mwaka 2019 alishtakiwa kwa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja na wanaume wengine wawili.

 

Wanaume hao wanasemekana kukutana kwenye mtandao wa Facebook kabla ya kupanga mkutano huko Kajiado ambapo, kulingana na polisi, walikubaliana kuwa mwalimu huyo alimlipia kila mmoja wa wanaume hao Ksh.elfu 10,000 kwa kitendo hicho cha ngono.

 

Hata hivyo Mwalimu huyo, hata hivyo, alishindwa kulipa kiasi kilichokubaliwa na kusisitiza kulipa nusu ya bei, hali iliyowafanya wanaume hao wawili wenye umri wa miaka ishirini kuripoti kisa hicho katika Kituo cha Polisi cha Kajiado.

 

Wote walikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa kufanya mapenzi ya jinsia moja ambapo kufikia sasa Kesi hiyo bado iko mahakamani.
Kesi hiyo itasikizwa Juni 6, 2023.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!