DJ Fatxo Aondolewa Mashtaka
Lawrence Njuguna, almaarufu DJ Fatxo leo hii Jumatano amefutiwa mashtaka ya mauaji katika uchunguzi wa kifo cha Jeff Mwathi.
Mahakama imeamuru uchunguzi ufanyike kwa kukosa ushahidi wa kutosha unaomhusisha na uchunguzi huo moja kwa moja.
Kupitia wakili wake Duncan Okatch, DJ Fatxo alikuwa ameandikia Idara ya Upelelezi na makosa ya Jinai (DCI) akiomba kuachiliwa kwa matokeo ya uchunguzi kuhusu kifo cha Jeff Mwathi.
Kulingana na Dj Fatxo ucheleweshaji huo uliharibu sifa na ustawi wake.