Home » Wanafunzi Kuchagua Vyuo Watakavyojiunga Navyo Kwa Wavuti.

Wanafunzi Kuchagua Vyuo Watakavyojiunga Navyo Kwa Wavuti.

Waziri wa elimu Ezekiel Machogu amezindua uteuzi wa vyuo vikuu kwa wanafunzi ambao walifanya mtihani wa KCSE mwaka jana.

 

Uteuzi wa wanafunzi kujiunga na vyuo vikuu unajiri wakati ambapo vyuo vikuu vinakabiliwa na mzigo wa deni la shilingi bilioni 61.1 jambo ambalo limeifanya serikali kubadili mfumo wa ufadhili wa vyuo vikuu.

 

Akizungumza wakati wa uzinduzi katika Chuo Kikuu cha Nairobi (UoN) Machogu amesema kuwa watahiniwa wote elfu mia 869,782 watastahiki kujiandikisha katika taasisi yoyote watakayo.

 

Aidha Machogu amesema kuwa watahiniwa elfu mia 173,127 waliopata la kuingia C+ watajiunga na kozi za shahada katika vyuo mbalimbali kote nchini.

 

Waliopata gredi ya C-plain na chini watafadhiliwa katika Vyuo vya Mafunzo ya Ufundi Stadi (TVET) kote nchini.

 

Waziri wa Elimu pia amesema kuwa taasisi zote tayari zimetimiza masharti yote yanayohitajika kusajili wanafunzi na tayari zimechapisha ada za kozi za programu tofauti za masomo kwenye tovuti zao.

 

Baada ya kuchaguliwa, Waziri Mkuu amesema, wanafunzi watapewa fursa ya kutuma maombi ya ufadhili wa masomo ya serikali kutoka kwa hazina ya Chuo Kikuu kulingana na mtindo mpya wa ufadhili uliotangazwa na Rais William Ruto.

 

Machogu ameongeza kuwa wanafunzi wasiopungua elfu 45,000 kutoka familia maskini watapata elimu ya chuo kikuu bila malipo kwani serikali itagharamia elimu yao kamili.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!