Home » Kenya Na Colombia Zashirikiana Kujenga Uhusiano Mwema Kibiashara

Kenya Na Colombia Zashirikiana Kujenga Uhusiano Mwema Kibiashara

Naibu Rais Rigathi Gachagua alimkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Colombia Francia Elena Marquez Mina, kwa mazungumzo ya pande mbili katika Makao yake Rasmi ya Karen, Nairobi.

 

Aidha, wamejadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

 

Jamhuri ya Kolombia imepiga hatua katika sekta ya kahawa na Kenya inatazamia kuingia katika ujuzi wa uzalishaji na uuzaji wa kahawa nje ya nchi huku ikitazama kuwa mdau mkuu katika sekta hiyo.

 

Viongozi hao wawili pia wamejadili kuhusu njia za kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa safari za ndege za kukodi moja kwa moja kutoka Kenya hadi Colombia ambazo zitakuwa kuwezesha biashara na uwekezaji.

 

Vile vile Viongozi hao wawili wamesimamia kutiwa saini kwa mikataba miwili ya maelewano ambayo itaimarisha ushirikiano wa kikazi kati ya Kenya na Colombia na pia kuimarisha usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake.

 

Naibu rais ameangazia utoaji wa msaada katika sekta ya afya na matumizi ya mianzi kama nyenzo ya bei nafuu ya makazi ambayo itasaidia sana serikali kufikia mpango wake wa makazi ya kijamii wa bei nafuu.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!