Home » Mpishi Wa Nigeria Hilda Baci Avunja Rekodi Ya Dunia

Mpishi wa Nigeria, Hilda Effiong Bassey, almaarufu Hilda Baci, amevunja Rekodi ya Dunia ya Guinness kwa ” upishi wa muda mrefu”.

 

Mpishi huyo mwenye umri wa miaka 27, Jumatatu asubuhi, alivunja rekodi ya saa 87 dakika 45 iliyowekwa na mshikilizi wa zamani wa rekodi ya dunia ya Guinness, Lata Tondon.

 

Hilda alizindua shindano hilo siku ya Alhamisi saa kumi kamili jioni alipoanza kupika na akaendelea kupikia mamia ya milo na kuwahudumia maelfu ya wateja katika upishu wa kihistoria wa siku nne.

 

Licha ya kuwa tayari amevunja rekodi hiyo, Hilda bado anaendelea na malengo yake ya kupika kwa saa 96 (saa 9 zaidi ya alivyokuwa amepanga awali) na kuweka rekodi mpya ya dunia ya kuwa binadamu wa kwanza duniani kutumia muda mwingi kupika.

 

Kwa zaidi ya saa 88, Hilda mrembo alipika, akipumzika kwa dakika 30 tu kisha akaendelea na lengo lake muda wote akiwa amesimama bila kulala.

 

Wakati wote huo, mfanyabiashara huyo maarufu wa mgahawa ameendelea kupokea wimbi la kuungwa mkono na maafisa wa serikali ya Nigeria, watu mashuhuri, makasisi, na Wanigeria wengine wenye nia njema ambao wengi wao walifika kwenye bustani ya Amore huko Lekki, Lagos ambako amekuwa akipika.

 

Asubuhi ya Jumatatu asubuhi, mamia ya wafuasi walifika ili kumtazama tu akipika.

 

Watu mashuhuri kama vile Banky W, Adesua Etomi, Charles Okocha, Tiwa Savage wote walifikia ukumbi wa kupikia huko Lagos ili kumuunga mkono na kumshangilia Hilda zaidi.

 

Kwenye Twitter, Burna Boy alishiriki picha yake, akitweet, “Nenda Hilda. Tunakutaka uvunje rekodi hiyo. Na ninaamini utaweza!”

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!