Home » Watu 6 Wafariki Dunia Katika Ajali Ya Barabara Sachangwan

Watu 6 wameaga dunia kutokana na ajali mbaya ya barabara katika eneo la Sachangwan, eneo bunge la Molo kaunti ya Nakuru usiku wa kuamkia leo Jumatatu.

 

Ajali hiyo inasemekana kuhusisha gari la matatu aina ya Eldoret Shuttle pekee ambalo lilikuwa linatoka mji wa Eldoret kuelekea jiji la Nairobi.

 

Naibu kamshina wa Molo Josphat Mutisya amedhibitisha ajali hiyo akisema kiini kamili cha ajali hiyo bado hakijabainika huku wakiwa na madai kuwa huenda dereva wa gari hilo alikuwa amelala na kupoteza mwelekeo.

 

Watu 12 ambao ni manusura wa ajali hiyo wanapokea matibabu katika hospitali ya Molo

 

Eneo la Sachangwan ni hatari sana kwa ajali ikizingatiwa kuwa watu zaidi ya 100 walipoteza maisha yao kutokana na ajali mbaya iliyotolea mwaka wa 2009, wakati wengi walipoteza maisha yao wakichota mafuta katika gari lililohusika na ajali hiyo na hatimaye likawaka moto.

 

Naibu kamshina Mutisya amewaomba madereva kuwa waangalifu zaidi na kuomba uongozi wa magari kuhakikisha kuna dereva wa ada hasaa katika safari za usiku na zile za masafa marefu ili kuzuia janga kama hili kutokea siku za usoni.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!