Home » Wamiliki Wa Matatu Watangaza Kupanda Kwa Nauli

Saa chache baada ya Mamlaka ya Kudhibiti Kawi na Petroli (EPRA) kuongeza bei ya mafuta, wamiliki wa matatu sasa wamedai kuwa nauli zitapanda kwa wasafiri wa masafa marefu kote nchini.

 

Akizungumza na wanahabari ,Branden Marshall afisa wa Chama cha Waendeshaji Matatu (A.M.O) amesema kuwa hii itaathiri abiria wanaosafiri kwenda eneo la Magharibi, Pwani miongoni mwa wengine kutoka katikatika mwa jiji la Nairobi (CBD).

 

Kulingana na Marshall hatua hiyo itawasaidia wawekezaji na washikadau kutokana na kuongezeka kwa bei ya mafuta ambayo inaathari uchumi.

 

Aidha ameongeza kuwa sekta ya matatu imebeba mzigo huo, akisisitiza kwamba walipaswa kushughulikia malengo, malipo ya bima, malipo ya wafanyakazi pamoja na kuhudumia mikopo mwishoni mwa mwezi.

 

Akipendekeza suluhu la hali hiyo, amebainisha kuwa serikali inapaswa kuweka mazingira mazuri kwa wafanyabiashara kwa kuweka mazingira ya kupata faida kwa pande zote zinazohusika.

 

Jana Jumapili, EPRA iliongeza bei za Super Petroli, Dizeli na Mafuta taa kwa Kshilingi 3.40 kwa lita, Kshilingi 6.40 kwa lita na Kshilingi 15.19 kwa lita mtawalia.

 

Jijini Nairobi, petroli inanunuliwa Kshilingi mia 182.70 kwa lita, Ksh168.40 kwa Dizeli na Mafuta ya Taa ilipanda hadi Kshilingi mia 161.13.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!