Home » Walimu Wakataa Nyumba Za Ruto Za Bei Nafuu.

Walimu waliojiunga na Muungano wa Walimu wa vyuo vya kadri (KUPPET) wamepinga mfumo wa hazina ya nyumba uliyoanzishwa na Rais William Ruto.

 

Wakati wakihutubia wanahabari, chama hicho kimesema kuwa baadhi ya wanachama wake tayari wanamiliki nyumba wakidai kwamba wanapaswa kutokatwa makato hayo ya asilimia tatu.

 

Zaidi ya hayo, wameteta kuwa muda ambao ungechukua kulipia nyumba zilizopendekezwa haukuwa wa kweli kwa walimu.

 

Baadhi ya wanachama wamesema haikuwa busara kuwataka waache nyumba zao za vijijini ambako wanafuga mifugo na kuishi katika ghorofa za juu na mbuzi, kuku na ng’ombe wao.

 

Kutokana na hali hiyo, wametoa makataa ya siku 14 kwa Tume ya Kuajiri Walimu (TSC) kuingilia kati na kuhakikisha walimu hatakatwa asilimia tatu iliyopendekezwa ambapo chama hicho kimetishia kugoma.

 

Jana Alhamisi raisRuto alitetea makato hayo akieleza kuwa wanasiasa pia wamekubali mfumo huo kwa kuona manufaa yake.

 

Kadhalika rais Ruto aliapa kuongeza idadi ya nyumba kutoka elfu 50,000 hadi elfu mia 200,000 kila mwaka kwa kushirikisha wawekezaji tofauti.

 

Hata hivyo, mnamo Jumatano, Aprili 25, Katibu Mkuu wa Makazi Charles Hinga alisisitiza kwamba makato hayo si ya lazima kwa Wakenya wote.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!