Home » ‘Yesu Wa Tongaren’ Kuzuiliwa Kwa Siku 4

Eliud Wekesa alias Yesu wa Tongaren|Photo Courtesy

Mhubiri Eliud Wekesa Simiyu, almaarufu Yesu wa Tongaren, ataendelea kuzuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Bungoma kwa siku nne zaidi hadi kukamilika kwa uchunguzi wa Kurugenzi ya Upelelezi wa Jinai (DCI).

 

Mahakama imetoa uamuzi huo leo hii Ijumaa ikisema kwamba ratiba hiyo itaruhusu wapelelezi wa DCI kukamilisha uchunguzi kuhusu Kanisa la Wekesa la New Jerusalem linalokabiliwa na madai ya mafundisho ya kidini yenye kutiliwa shaka.

 

Awali upande wa mashtaka uliomba mhubiri huyo mwenye utata azuiliwe kwa siku saba ili kutoa nafasi ya uchunguzi kuhusu nyumba yake na tabia yake binafsi.

 

Hata hivyo, Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Bungoma Tom Mark Olando amekanusha ombi hilo badala yake akaagiza upande wa mashtaka kufanya uchunguzi ndani ya siku nne.

 

Maafisa wa Polisi wanatarajiwa kutumia ratiba iliyotajwa ya Wekesa ambayo walisema inaaminika kuwa eneo la uhalifu, kanisa lake na pia kumpima mhubiri huyo kiakili.

 

Kesi hiyo itatajwa Mei 16, 2023.

 

Kulingana na madai yaliyowasilishwa na Afisa Mpelelezi Elijah Acharia jana Alhamisi, ‘Yesu Wa Tongaren’ anakabiliwa na mashtaka yakiwemo ya itikadi kali, utakatishaji fedha, kumiliki au kutumia mapato ya uhalifu na kusimamia jamii isiyo halali.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!