Home » KRA Yamwokoa Mchungaji Ezekiel Odero

Mamlaka ya ushuru nchini (KRA) imethibitisha kwamba kanisa la New Life Prayer Center la Ezekiel Odero limekuwa likiwasilisha marejesho ya kodi, na hivyo kuondoa shaka kuhusu utiifu wake wa sheria.

 

Leo hii Alhamisi, Msajili wa Vyama Jane Joram amewaambia maseneta kwamba kanisa la Mchungaji Ezekiel na kanisa la Good News International la Mchungaji Ezekieli Paul Mackenzie walipewa notisi ya siku 30 kuonyesha sababu za kwa nini makanisa yao yanapaswa kufungwa kwa kushindwa kufuata baadhi ya kanuni za uongozi wa makanisa notisi ambayo anasema ilitolewa tarehe 27 Aprili.

 

Msajili huyo ameonyesha kuwa kanisa la Mackenzie liko hatarini kufungwa kwani malengo yake huenda yakatumiwa kwa madhumuni yasiyo halali na, kwa hivyo, hayapatani na sheria za Kenya.

 

Kanisa la Mchungaji Ezekiel linakabiliwa na kufungwa kwa kushindwa kuwasilisha marejesho ya kodi kwa muda wa miaka 10 iliyopita.

 

Tayari anapigania mahakama kuzuia akaunti za benki na M-Pesa, ambazo ni zaidi ya 35, na kurejeshewa kituo chake cha televisheni cha World Evangelism huku uchunguzi kuhusu mauaji ya Shakahola ukizidi.

 

Jana Jumatano, Mahakama Kuu ya Mombasa ilimruhusu Mchungaji Ezekiel na wafuasi wake kuingia katika majengo ya kanisa hilo eneo la Mavueni Kaunti ya Kilifi, pamoja na huduma zisizokatizwa kisheria.

 

Jaji wa mahakama ya Mombasa Olga Sewe alitoa maagizo hayo baada ya mwinjilisti huyo kulalamikia ugumu aliokuwa akikumbana nao kuendesha ibada kutokana na kuwepo kwa polisi wengi humo.

 

Ikumbukwe kwamba Mamlaka ya Mawasiliano ya Kenya (CA) ilisitisha shughuli za kituo cha televisheni na kanisa lililoko Mavueni Hii ilikuwa baada ya Mchungaji Ezekiel kukamatwa na kufikishwa mahakamani kutokana na mauaji ya Shakahola ambayo yamegharimu maisha ya watu 130.

 

Hata hivyo, aliekea Mahakama Kuu kubatilisha uamuzi huo kupitia timu ya mawakili wanane akiwemo Jared Magolo, Cliff Ombeta, Danstan Omari, Shadrack Wambui, Brian Okoko, na Duncan Osoro.

 

Mchungaji Ezekiel ametaja tuhuma dhidi yake kuwa hazina uthibitisho na ambazo kashfa si za kweli, na kukana kuhusika na mauaji ya umati wa Shakahola na kushirikiana na Mackenzie.

 

Vile vile Amedai kuwa kufungia akaunti zake za benki kumemnyima bila sababu yeye na waumini wake uhuru wa kuabudu na haki ya kumiliki mali kama ilivyoamriwa katika katiba.

 

Kwa mujibu wa Mchungaji Ezekiel, kufungiwa kwa akaunti za benki za kanisa hilo ni sehemu ya njia kinyume na katiba ambayo Serikali imechukua kukatiza huduma yake licha ya kujua kuwa hana hatia ya madai yoyote kuhusu mauaji ya Shakahola.

 

Kwa sasa amewashtaki Mwanasheria Mkuu Justin Muturi, Inspekta Mkuu wa Polisi Japheth Koome, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma, mamlaka ya mawasiliano CA na afisa wake mkuu Ezra Chiloba, na wizara ya Mambo ya Ndani kwa kundelea kumkandamiza licha ya kuonekana kuwa hana hatia.

 

Shirika la Kurejesha Mali, Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi EACC na Baraza la Kitaifa la Makanisa la Kenya NCCK ni miongoni mwa wahusika.

 

Mackenzie na Mchungaji Ezekiel wanachunguzwa kwa makosa ya mauaji, utekaji nyara, itikadi kali, uhalifu dhidi ya ubinadamu, ukatili wa watoto, ulaghai na utakatishaji fedha haramu.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!