Home » Yesu Wa Tongaren: Ninahubiri Injili Ya Kweli Msinitie Nguvuni

Yesu Wa Tongaren: Ninahubiri Injili Ya Kweli Msinitie Nguvuni

Mhuburi mashuhuri anayejulikana kama Yesu wa Tongaren amewasihi maafisa wa polisi wasimkamate baada ya kutarajiwa kujisalimisha katika makao ya idara ya uchunguzi na upelelezi DCI tawi la Bungoma, akishikilia kuwa anahubiri injili ya ukweli pekee.

 

Kamanda wa polisi wa Bungoma Francis Kooli amemtaka Eliud Wekesa kufika kuhojiwa huku ukaguzi wa mashirika ya kidini ulioamriwa na serikali ukizidi kushika kasi kufuatia uchukuaji wa miili zaidi ya mia 100 kutoka msitu wa Shakahola ukiendelea.

 

Waziri wa Mambo ya Ndani Kithure Kindiki wiki jana alipuuzilia mbali madai kwamba serikali inanuia kuanzisha vita dhidi ya taasisi za kidini, akifafanua kwamba lengo kuu limegeuzwa kuwaondoa viongozi wa dini walaghai wanaoendeleza itikadi kali na uhalifu.

 

Kindiki alikariri kuwa serikali haijakatishwa tamaa na kelele hizo na itaendelea kulenga kuwawinda wale wanaotumia vibaya ushawishi wa kidini kwa nia potofu, akitaja mkasa wa Shakahola kama ushahidi wa vurugu kubwa na unyanyasaji wa kiroho ambao serikali inataka kuepusha wakenya kwayo.

 

Wakati wa misa iliyoandaliwa na Parokia ya Chaaria huko Meru kusaidia watoto wenye ulemavu, Waziri Mkuu alitambua mchango mkubwa wa taasisi za kidini katika maendeleo ya kijamii na usimamizi wa usalama wa Kenya.

 

Hata hivyo, alionya kuwa serikali haitasita kuondoa mafundisho yasiyo ya kawaida na shughuli haramu zinazojificha kwa kisingizio cha uhuru wa kidini.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!