Home » Harmonize Apata Mpenzi Mpya

Harmonize

 

Makali wa kibao cha Single Again Harmonize ameuaga upweke baada ya kumtambulisha mwanamke mwenye asili ya nchini Rwanda anayejulikana kwa jina la Phiona kuwa ndiye ua la moyo wake kwa sasa.

 

SOMA PIA:Harmonize Amchumbia Esma Platnumz

 

Kupitia ukurasa wa Instagram, Harmonize alishindwa kuficha penzi hilo na mpenzi wake mpya Phiona kulianika hadharani kwa kuweka picha ya mrembo huyo Instastory na kueleza ya kuwa hayuko Single tena.

 

 

Taarifa hizi zimejiri miezi michache baada ya msanii huyo kutangaza  kuwa yuko Single baada ya kuachana na muigizaji kutokea Tanzania Kajala Masanja baada ya tuhuma za kuwepo kwa uongo katika penzi lao.

 

 

Sambamba na kuachana na Kajala, Harmonize aliachia kibao chake cha Single Again na kueleza ya kuwa wimbo huo umechochewa na penzi lake lililopita lililomuumiza na kuamua kuandika wimbo huo.

 

 

Baada ya kuachana na Kajala, Tembo alihushwa na tuhuma mbalimbali za kuwa kwenye mahusiano na watu mbalimbali kama vile dada wa Diamond, Esma Platnumz pamoja na mwanamuziki Fezza Kessy.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!