Home » NTSA Yazindua Msako Wa Kitaifa

Mamlaka ya Kitaifa ya Uchukuzi na Usalama barabarani (NTSA) leo hii Jumatatu imeanza msako wa kitaifa dhidi ya magari ambayo yanakiuka Sheria na Kanuni za Trafiki.

 

Katika oparesheni hiyo, iliyoanza majira ya asubuhi watoto waliporipoti kurejea shuleni, maafisa waliotoka katika mashirika mbalimbali waliweka vizuizi barabarani na kuwataka madereva kutoa hati rasmi ili kuchunguzwa na kuthibitishwa.

 

Sehemu ya msako mkali uliopewa jina la ‘Kliniki ya Usalama Barabarani’, madereva wa magari walitarajiwa kutoa vitambulisho vyao vya Taifa kwa madereva na makondakta pamoja na leseni zao halali.

 

Msako huo umetokana na agizo la Waziri wa Uchukuzi Kipchumba Murkomen ambapo aliamuru mamlaka hiyo kuhakikisha kuwa magari ya kibinafsi na ya utumishi wa umma yanafuata Sheria.

 

Mnamo Jumatano, Aprili 19, Murkomen alitoa maagizo mawili kwa NTSA na wakuu wa shule baada ya ajali mbaya kuwaua wanafunzi sita katika barabara kuu ya Nairobi-Nakuru, akibainisha kuwa hakuna usafiri wa shule utakaoruhusiwa kuhudumu kati ya saa 10 USIKU na 5 asubuhi kama ilivyobainishwa katika Sheria ya Trafikiya 2017.

 

Waziri Murkomen pia aliitaka NTSA kuhakikisha kuwa watoto wote wanaokwenda shule wametengewa viti vilivyo na mikanda ya usalama na lazima wawe wamefungwa kila wakati.

 

Kujibu, NTSA ilisema kuwa magari ambayo hayatii Sheria yatapigwa marufuku, kuhifadhiwa na kuwasilishwa kwa ukaguzi ili kufuata sheria katika kituo cha ukaguzi cha NTSA.

 

Mamlaka hiyo ilieleza zaidi kuwa zoezi la ‘Kliniki ya Usalama’ la ukaguzi wa magari hayo yakiwa barabarani litahakikisha maisha ya wasafiri wakiwemo watoto wanaokwenda shule yanakuwa salama.

 

Kliniki ya Usalama pia ilikuwa ikitathmini mabadiliko ya tabia na mtazamo miongoni mwa watumiaji wa barabara na kuboreshwa kwa uzingatiaji wa usalama barabarani kwa magari ya umma… yale kibiashara na waendesha Boda Boda.

 

Kadhalika NTSA pia imebainisha kuwa ilikuwa katika ushirikiano ulioimarishwa na washikadau kadhaa katika usimamizi wa usalama barabarani.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!