Uhuru Apaza Sauti
Aliyekuwa Mbunge wa Nyeri Mjini Wambugu Ngunjiri ameangazia sababu tofauti za machafuko yaliyokumba chama cha Jubilee akibainisha kuwa kuna hatua ambazo rais wa zamani Uhuru Kenyatta anaweza kuchukua.
Kulingana na Ngunjiri, Uhuru alifikia kilele cha maisha yake ya kisiasa na hangeweza kuvuka hatua hiyo kwani aliwahi kuwa Mkuu wa Nchi na anadai ni vyema ajiweke kando na kuwaacha watu wengine waongoze chama ili kuepusha lawama kutoka kwa wananchi.
Zaidi ya hayo, amesema kuwa Uhuru huenda asiweze kushughulikia hatua inayohitajika ili kuhakikisha chama kinaendelea kukua kwa sababu tayari alikuwa amechagua upande upinzani.
Kulingana na Ngunjiri, timu moja katika Jubilee inaamini kwamba njia ya kufuata ni kukanusha uchaguzi uliopita na kuiondoa serikali iliyopo madarakani huku timu nyingine ikikubali ukweli wa kuwa na serikali ya Kenya kwanza na kusonga mbele.
Mbunge huyo wa zamani amesema kuwa wanachama wa Jubilee mara nyingi hawakujumuishwa kwenye mikutano na kongamano la wanahabari lililofanywa na muungano wa Azimio na kubainisha kuwa ni wabunge waliowakilisha chama na iwapo wabunge wa jubilee hawakujitokeza basi ilionyesha hawakuwa na mshikamano.
Ngujiri pia ameibu madai ya kuwa wanachama wa chama cha Jubilee waliachwa nje ya orodha ya wawakilishi ambao wangewakilisha muungano wa Azimio kwenye mazungumzo ya pande mbili.
Pande mbili zinadai uongozi wa chama tawala cha zamani una jukumu la kufanya…. Mmoja ukiongozwa na Jeremiah Kioni na mwingine Kanini Kega.
Rais mstaafu Kenyatta amekumbwa na utata baada ya mrengo wa Kega kumteua Sabina Chege kama kiongozi wa chama akichukua nafasi ya Uhuru Kenyatta.
Katika kurejea, Kioni alifuta uanachama wa Kega na Chege, na hivyo kuchochea mgawanyiko ndani ya chama hicho kikuu cha zamani.
Hata hivyo, Chege alipata afueni Bungeni baada ya Spika Moses Wetangula kuupa muungani wa Azimio siku 30 kabla ya wao kuchukua nafasi yake kama naibu kinara wa muungano huo.