Gachagua Adokeza Mpambano Kati Ya Ruto,Raila
Naibu Rais Rigathi Gachagua amedai kuwa kuna mapambano kati ya Rais William Ruto na kiongozi wa Azimio Raila Odinga, ambayo huenda yakafanyika wakati wa hafla ya maziko ya marehemu Mukami Kimathi.
Akizungumza wakati wa ibada fupi Mukami Kimathi, Gachagua amefichua kuwa Ruto atahudhuria mazishi hayo yanayotarajiwa kufinyika Jumamosi, Mei 13.
Haya yanajiri saa chache baada ya Raila kuthibitisha kuhudhuria kwake alipozuru Lee Funeral Home ambapo mwili wa Mukami ulikuwa umehifadhiwa.
Katika kujibu madai ya awali ya Raila kwamba hakuna mtu ambaye angemzuia kuhudhuria mazishi hayo, Gachagua amesema kuwa kila mtu anakaribishwa katika boma la KIMATHI.
Katika hatua ambayo inaweza kuwa ya wasiwasi, Gachagua amedai kuwa mazishi ya Mukami yangetoa jukwaa la kujadili dhuluma za ardhi ambapo kwa muda mrefu sula hilo limekuwa likifungiwa macho na viongozi mbalimbali.
Mazishi ya Mukami yatakuwa mara ya kwanza kwa Raila Odinga kushiriki jukwaa moja na na Rais William Ruto na Naibu wake tangu uchaguzi wa urais wa Agosti 9, 2022 uliokumbwa na utata.