Home » Biography: Fahamu Wasifu Wa Beda Andrew

Ukitaja orodha ya wasanii wa Injili ambao wanatamba sana nchini Tanzania kwa sasa bila shaka jina “Beda Andrew” halitakosekana na hii ni kutokana na jinsi ambavyo ameweza kuteka kundi kubwa la vijana kuweza kufuatilia muziki wa Injili. Huu hapa ni wasifu ya msanii wa nyimbo za injili Beda Andrew (Biography) kutoka Tanzania.

 

Beda Andrew ni hodari, na unaweza ukathibitisha hilo kupitia nyimbo zake kama “Mambo Yatakuwa Sawa”, “Mbali Sana” na hata “Daima Milele” ambao ni wimbo wake wa hivi karibuni.

 

SOMA PIA:Makala: Mambo 5 Usiyoyajua Kuhusu Msanii Cherry

Kupitia makala unaweza kumfahamu zaidi msanii huyu ambaye kando na kipaji chake cha kuimba pia ni mchoraji mzuri sana. Hii hapa ni Biography/ Wasifu wa Beda Andrew kutoka nchini Tanzania

 

Maisha Kabla Ya Muziki

Beda ametokea kwenye familia ya kikristo na katika moja ya mahojiano aliyoyafanya nyuma kidogo, msanii huyo alidokeza kuwa baba yake ni Mchungaji.

 

 

Nguli huyu wa muziki wa Injili amezaliwa jijini Dar Es Salaam na amekulia eneo la mji mwema huko Kigamboni.

 

Kutokana na kuhudhuria sana kanisani pindi akiwa mtoto, Beda Andrew alijiunga na Sunday School kama muimbaji na hapo ndipo kipaji chake cha muziki kilichipua.

 

Kando na kuimba, Beda alielezea kuhusu kipaji chake cha uchoraji kilichoanzia shule ya Sekondari Azania. Mara nyingi alikuwa anafundishwa kuhusu sanaa ya uchoraji.

SOMA PIA:TECH: Here An App Where People Don’t Post Memes

 

Wasanii Anaowatazama

Akiwa kwenye mahojiano na Huruma Charles, Beda alidokeza kuwa anavutiwa sana na mwanamuziki kutoka nchini Marekani. Alimtaja Kirk Franklin ni moja ya wasanii hodari sana wa Injili nchini humo wanaomvutia.

 

Aidha aliongeza kwa kusema kuwa Malkia wa muziki wa Injili, Rose Muhando ni moja kati ya wasanii ambao alikuwa anawasikiliza sana pindi akiwa mtoto.

 

Kushiriki Mashindano

Katika harakati za kujitafuta na kuvumbua kipaji chake, Beda mwaka 2016 alishiriki kwenye mashindano ya Gospel Star Search na aliweza kufanya vizuri kwenye mashindano hayo.

 

Aidha, kabla ya hapo, Beda alidokeza kuwa mara yake ya kwanza kabisa kuingia studio ili kuwa ni mwaka 2014. Huu ulikuwa mwaka ambao msanii huyo alirekodi wimbo wake wa kwanza.

 

Kitu kingine usichokijua kuhusu wasifu au biography ya Beda Andrew ni kwamba Februari mwaka 2022, aliandika historia mpya kwenye muziki wake. Jambo hili limejiri baada ya kuachia album yake ya kwanza ya iliyopewa jina la “Kweli” yenye nyimbo 13. Baadhi ya nyimbo zilizomo kwenye album hiyo ni pamoja na Happy Happy, Upande Wangu na nyinginezo nyingi.

 

Kwenye mtandao wa Boomplay, Kweli tayari imeshakusanya streams zaidi laki mbili. Kwa sasa tayari Beda ameshafanya video ya baadhi ya nyimbo zilizomo kwenye albamu hiyo.

Tuzo Ya Maranatha

Moja kati ya nyakati za kukumbukwa kwenye historia ya muziki wa Beda Andrew ni pale aliposhinda tuzo za Maranatha. Huu ulikuwa ni ushindi maalum kwa watumishi na waimbaji wa muziki wa Injili hapa Afrika Mashariki.

 

Tuzo ya Maranatha ni tuzo ya kwanza kabisa kwa Beda Andrew kushinda. Baada ya kushinda tuzo hiyo aliweza kukutana na wasanii wakubwa wa Injili Tanzania na kukuza zaidi jina lake.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!