Home » Rais Ruto, Kishida Fumio Kufanya Mazungumzo

Rais William Ruto atafanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Japan Kishida Fumio leo Jumatano katika Ikulu ya Nairobi.

 

Waziri Mkuu Kishida Fumio aliwasili nchini jana Jumanne na kupokelewa na Waziri wa Masuala ya Kigeni Alfred Mutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta JKIA.

 

Waziri Mkuu wa Japan yuko katika ziara ya kiserikali ya siku mbili.

 

Viongozi hao wawili wanatarajiwa kufanya mazungumzo baina ya nchi hizo mbili kuhusu kuimarisha zaidi uhusiano kati ya Kenya na Japan, kuimarisha uratibu wa masuala ya kikanda na kimataifa na kukuza ukuaji wa Afrika katika biashara.

 

Fumio pia anatazamiwa kukutana na jumuiya ya wafanyabiashara wa Japani, vijana wa kujitolea na wanaoanzisha biashara.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!