Home » Diamond Awapiku Wasanii Wa Afrika

Msanii wa muziki wa kizazi kipya wa Bongo Fleva kutoka nchini Tanzania Diamond Platnumz amewashangaza na kuwakanyaga wasanii wa Nigeria baada ya kuwabwaga wote kwa mujibu wa takwimu za mtandao wa YouTube.

 

Msanii huyo aliyetua nchini Ujerumani kwa ajili ya shoo yake kubwa Jumamosi hii alipakia takwimu mpya zinazowaonyesha wasanii wa bara la Afrika na jinsi wanavyotumbuiza jukwaani.

 

Kwa mujibu wa takwimu hizi, Diamond ndiye msanii wa Kiafrika ambaye nyimbo zake hutolewa zaidi kwenye jukwaa hilo.

 

Tangu aanze muziki zaidi ya miaka kumi iliyopita, Diamond ndiye msanii maarufu zaidi kwenye YouTube aliyetazamwa mara bilioni 2.14.

 

 

Wasanii kutoka Nigeria na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wameshika nafasi ya pili huku Burna Boy kutoka Nigeria akimkaribia Diamond kwa kutazamwa mara bilioni 2.05 kwenye YouTube.

 

Wizkid ametazamwa mara bilioni 1.67 kwenye YouTube huku Fally Ipupa, msanii wa kizazi kipya wa Rhumba kutoka DRC akishika nafasi ya nne kwa kutazamwa mara bilioni 1.40 na Davido ambaye anazidi kutamba na albamu yake mpya ya Timeless alishika nafasi ya tano bora kwa kutazamwa mara bilioni 1.29.

 

Diamond amekuwa akijitahidi kwenye jukwaa hilo licha ya dhana kuwa wasanii wengi hasa kutoka nchi za Magharibi hawazingatii sana takwimu zao kwenye mtandao wa YouTube kwa sababu inasemekana mapato ya jukwaa hilo bado ni madogo sana.

 

Kwa sababu hiyo, wasanii wengi sasa wanawekeza muziki wao katika majukwaa mengine kama Boomplay, Audiomac, Spotify na mengine ambayo kwa kawaida hayapangi video na mapato yao ni ya ushindani zaidi kuliko ya YouTube.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!