Home » Harmonize Amchumbia Esma Platnumz

Mwanamuziki Harmonize ameingia tena katika vichwa vya habari mara baada ya taarifa kusambaa zikimuhusisha kuwepo katika mahusiano ya kimapenzi na mfanyabiashara Esma Platnumz.

 

Ujio wa taarifa hizo ni baada ya Harmonize kumtaja Esma kuwa ndiye aliyeshiriki kuingiza sauti katika wimbo wa Say Yes ambayo Jeshi ameshirikishwa na Dj Seven na baadaye kufuta chapisho Hilo katika ukurasa wake wa Instagram

 

SOMA PIA: Harmonize Ataja Siri Ya Uandishi Wa Kazi Zake

Esma ambaye pia ni dada wa msanii Diamond Platnumz amezikana habari hizo na kuweka wazi ya kuwa yeye na Harmonize ni washkaji tu na hakuna lolote ambalo linaendelea kati yake na Harmonize.

Pia katika wimbo wa Say Yes Esma ameeleza ya kuwa ni hatua ya kuwashika mkono wasanii wa Bongo na siyo kama wao wanavyosema watu. Kwa mujibu wa Bongo 5, jambo hili lilimganya Esma atoke Instagram alipoingia live mara baada ya mashabiki zake kuhitaji taarifa juu yake na Harmonize endapo ni za kweli.

 

https://www.instagram.com/reel/CrihuBCu3qX/?igshid=YmMyMTA2M2Y=

Harmonize pamoja na Esma ni marafiki walioanzia uhusiano huu tangu kipindi ambacho Harmonize akiwa WCB Wasafi hivyo kitendo hicho cha kuhusishwa na mahusiano kinaweza kuwepo kutokana na uhusiano wao wa kipindi cha nyuma wakiwa kama washkaji.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!