Home » Kondoo Walioibwa Northlands Wapatikana Juja

Kondoo tisa aina ya Dorper walioibwa kutoka kwa shamba la aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta linalomilikiwa na familia ya Northland mwezi mmoja uliopita wamepatikana katika eneo la Mugutha, Kaunti Ndogo ya Juja.

 

Wanyama hao ambao walionekana dhaifu na wenye njaa walipatikana katika nyumba ya kifahari wakati wa msako wa polisi dhidi ya pombe haramu.

 

Kamanda wa Polisi wa Kaunti Ndogo ya Juja Phylis Muthoni amelazimika kuwalisha kwanza kwa kutumia majani mabichi ya miti katika lake boma kabla ya familia ya uhuru kuarifiwa.

 

Meneja wa shamba la Northlands, ambaye alikuwa ameandamana na baadhi ya wafanyakazi wake, alifika nyumbani hapo, na kuwatambua kondoo hao na kuwachukua baada ya kurekodi taarifa katika Kituo cha Polisi cha Mugutha.

 

Aidha Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Kiambu Perminius Kioi ambaye aliongoza uvamizi huo haramu wa pombe alisema mmiliki huyo atachukuliwa kuwa mwizi wa kawaida wa mifugo.

 

Mmiliki wa nyumba hiyo alikuwa ametoweka baada ya kuhisi hatari lakini Kioi alisema wanamfuatilia.

 

Hii si mara ya kwanza kwa kondoo zaidi ya 1,500 walioibwa katika shamba la Northlands Machi 27, mwaka huu kupatikana sehemu mbalimbali huku mamia ya mifugo hao wakirudishwa shambani na wezi hao ambao walidai wanahofia laana.

 

Katika nyumba hiyo, mamia ya pombe ghushi zilizokuwa zimepakiwa kwa ajili ya kusambazwa, baadhi zikiwa na majina ya chapa zinazofahamika zilitwaliwa.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!