Home » DJ Seven Aachilia Album Yake Ya Kwanza
DJ Seven Let Love lead

 

Dj maarufu na mzalishaji wa muziki anayejulikana kwa jina la Dj Seven ameachilia Albamu yake ya kwanza aliyoipa jina la Let love lead ambayo amewashirikisha wasanii kedakede kutoka ndani na nje ya Tanzania.

 

SOMA PIA:Takriban Wakenya Wamekwama Nchini Sudan  Alfred Mutua

 

Katika uzinduzi wa Albumu hiyo Dj Seven alianza kwa kuwaita waandishi wa habari siku ya Jumatano mchana tarehe 27 mwezi wa nne. Katika kusanyiko hilo  Seven alitangaza ujio wa kazi hiyo ikiwa imesheheni jumla ya ngoma 14.

 

DJ Seven

Let Love Lead ni muunganiko wa nyimbo za mahaba yenye kusherehesha mapenzi. Dj Seven katika muunganiko huo amefanikiwa kuunganisha sauti za wasanii mbalimbali barani Afrika akiwemo Harmonize, Ibraa, Jovial, Jaywilly, Dayoo, Spice Diana, Skales pamoja na wengine wengi.

 

Hii ni kazi ya kwanza kwa Seven na moja kati ya mambo ambayo  anastahili kujivunia kwa kukamilisha kazi hiyo yenye ngoma kama vile Sababu, Trust, Only you, Napenda pamoja na Say yes akipita nayo Harmonize.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!