Wanaharakati Wadai Serikali Inaficha Uovu Shakahola (video)
Kundi la wanaharakati kutoka shirika la MUHURI sasa linaikashifu serikali kwa kile wanachodai ni kujaribu kuficha hali halisi ya uovu na maafa yanayofukuliwa Shakahola kaunti ya kilifi.
Wanasema hatua ya kuzuia wanaharakati na wanahabari kushuhudia shughuli ya ufukuzi inaleta tumbo joto na kuzua shauku miongoni mwa wakenya
Mkurugenzi mkuu wa bodi ya MUHURI Africa Kelef Khalifa anadai huenda Msitu huo wa shakahola ulitumika na serikali kuzika miili ya baadhi ya watu walioshukiwa kuuawa na polisi kwa kisingizio ya Ugaidi.
‘’Tunashuku, kati ya makaburi hayo ya shakahola, kuna makaburi ya watuhumiwa wa ugaidi ambao walizikwa takibani miaka miwili au mitatu iliyopita. Kwa hivyo wanahofia iwapo watafukua na DNA ibaini si ya dini hiyo, basi huenda ikazua hofu na maswali mengi sana nchini na dunia’’ Alisema Khalifa
Khalifa ameshangaa ni kwa nini serikali imebadili nia yake na kufanya ufukuzi wa miili katika msitu huo ambao umegeuzwa kuwa oparesheni ya siri. Kutokana na hayo shirika hilo linamtaka Waziri Kindiki kuweka mambo parawanja ili kuondoa wasiwasi katika taifa
Serikali siku ya jumatano kupitia waziri wa usalama Prof Kindiki Kithure lilitangazi amri ya kutotoka nje kwa siku thelathini maeneo ya Chakama, ambayo inamiliki msitu wa shakahola,na kuwa ruhusu maafisa wa polisi na waendeshaji wa uokoaji na ufukuzi kuingia maeneo hao. Wanaharakati, wanahabari na mashirika megine yalikatanzwa kuingia katika msitu huo amabayo imetangazwa kuwa hatari kwa usalama
Tayari Mshukiwa mkuu wa maovu hayo, kasisi tata Paul Mackenzie anazuiliwa na polisi na vile vile mhubiri mwingine Ezekiel Odero amekamatwa na kuhojiwa na DCI