Home » Mwanamke Wa Bungoma Afariki Akielekea Kilifi Kwa Maombi

Two big burning candles. Bright light on dark background. RIP darkness template. Birthday party. Romantic evening on Valentine.

Mwanamke mmoja ambaye alikuwa akisafiri kutoka Bungoma kuelekea Mombasa kutafuta maombi amefariki akiwa ndani ya basi.

 

Ripoti ya polisi ambayo iliwasilishwa katika Kituo Kikuu cha Polisi na dereva wa basi la Simba kocha Musa Moi Owalo amesema kuwa Consolota Wesonga Otieno alikuwa akisafiri kutoka Bungoma kuelekea Mombasa alipofariki njiani.

 

Kulingana na bintiye Faith Otieno, mamake aliondoka Bungoma kuelekea Kilifi kutafuta maombi kwa vile amekuwa akiugua kwa muda.

 

Otieno alibainisha kuwa ilikuwa ni bahati mbaya kwamba mamake aliacha kutumia dawa zake na kuanza kumfuata anayedaiwa kuwa pasta kwenye matangazo ya televisheni.

 

Mwili huo umepelekwa hadi katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Coast General, ukisubiri kufanyiwa upasuaji

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!