Home » Elachi: Familia Ya Mackenzie Na Wasimamizi Pia Wakamatwe

Elachi: Familia Ya Mackenzie Na Wasimamizi Pia Wakamatwe

Beatrice Elachi Biography: Age, Party, Qualifications, Children, Parents, Photo - The SagaBeatrice Elachi, Mbunge wa Dagoretti Kaskazini, amedai kwamba wanafamilia wa kasisi mwenye utata Paul Mackenzie, pamoja na wasimamizi wake wa kanisa, wanapaswa kukamatwa.

 

Kasisi huyo mwenye utata anayeongoza kanisa la Good News International anachunguzwa baada ya mamlaka kugundua maiti za wafuasi wake zikiwa zimezikwa katika Msitu wa Shakahola huko Kilifi.

 

Uchunguzi umeefichua kwamba Mchungaji Mackenzie alidaiwa kuwaagiza washiriki kujinyima kula na kufaa njaa ili “kukutana na Yesu.”
Kulingana na Mbunge Elachi, wasaidizi wa karibu wa Mackenzie walimtia moyo kutekeleza vitendo vyake vya uhalifu na wanapaswa kuwajibishwa pia.

 

Amedai kuwa wasimamizi hao walikuwa na jukumu la kuhakikisha kuwa wafuasi wa ibada hiyo wangefunga.

 

Mbunge huyo pia amedai kuwa wahasiriwa walishawishiwa kwa urahisi kufuata fundisho la mchungaji Mackenzie kwa sababu walitoka katika mazingira duni na walikuwa wamekata tamaa.

 

Kulingana na nae sheria kali zaidi zinazosimamia usajili wa vyama vya kidini nchini Kenya zinafaa kutekelezwa, akibainisha kuwa viongozi wengi wa kidini huishia kuwalaghai waumini kwa manufaa ya kibinafsi.

 

Kufikia sasa, polisi wanasema wamewakamata waumini kumi na wanne wa ibada hiyo, wawili kati yao ni kakake Mackenzie na mkewe, kulingana na mwathiriwa ambaye anasema aliwaona kwenye televisheni baada ya kunaswa.

 

Aidha, Japhet Koome, Inspekta Jenerali wa Polisi, aliwaambia waandishi wa habari mchana kuwa watu 29 wameokolewa wakiwa hai.
Mackenzie alishtakiwa mwezi uliopita baada ya watoto wawili kufa kwa njaa wakiwa chini ya uangalizi wa wazazi wao na yuko kizuizini.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!