Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta Awasili Ethiopia
Rais mstaafu Uhuru Kenyatta amewasili nchini Ethiopia kujadili maendeleo ya amani na usalama nchini humo.
Katika taarifa iliyotolewa kupitia Ofisi ya Rais….rais huyo wa zamani amebainisha kuwa alisafiri kama Mjumbe wa Amani wa Kenya nchini Ethiopia.
Viongozi wengine wa Afrika wamejiunga na Kenyatta, akiwemo Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo na aliyekuwa Naibu Rais wa Afrika Kusini Phumzile Mlambo.
Pia amekutana na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) Moussa Faki katika makao makuu ya AU.
Kenyatta ameongoza AU na Jopo lake la Ngazi ya Juu kuwezesha mazungumzo ya amani ambayo yalishuhudia serikali ya Ethiopia na chama cha Tigray People’s Liberation Front (TPLF) kutia saini mkataba wa amani mnamo Novemba 2022.
Serikali ya Ethiopia na hasimu wa chama cha Tigray People’s Liberation Front (TPLF), kinachodhibiti eneo la kaskazini la Tigray, walikubaliana kuhusu mkutano wa pili mjini Nairobi kujadili awamu ya pili ya mazungumzo.