Home » Saida Mouh Akana kufahamu Umiliki Wa Mali Za Achraf Hakimi

Saida Mouh, Achraf Hakimi

 

Sakata linalomuhusu mchezaji wa soka wa timu ya PSG, Achraf Hakimi limechukua sura mpya baada ya mama yake mzazi Saida Mouh kufanya mahojiano na kituo kimoja cha habari nchini Morocco.

 

SOMA PIA:Achraf Hakimi’s Wife Surprised He Owns Nothing

 

Katika mahojiano hayo aliyoyafanya Saida Mouh aligusia kwa ukubwa suala la mwanae kumpatia umiliki mkubwa wa mali zake lakini kwa mujibu wake mama huyo alijitetea na kusema hakuwa akijua kama mwanae alifanya hivyo. Alisema

 

….Sikuwa nikifahamu. Tatizo ni nini ikiwa habari ni za kweli? Mwanangu asipofanya hivi hataweza kumuondoa mwanamke huyo …..

 

Saida Mouh x Achraf Hakimi

Saida ambaye amekuwa akionekeana zaidi na mwanae huyo ameoneshwa kutokwazika na jambo la mwanawe huyo la kumpatia umiliki huo wa mali bila ya mkewe wala yeye mwenyewe kufahamu suala hilo.

 

Achraf Hakimi pamoja na mkewe Hiba Habouk wako mbioni kutalakiana na suala hilo likichochewa na kesi iliyokuwa ikimuandama beki huyo wa timu ya Taifa ya Morocco kwa madai ya ubakaji wa mwanamke wa miaka 24.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!