Home » Shilole Ajikita Kuwekeza Katika Ardhi

 

Mwanamziki na mjasiriamali Zuwena Mohammed, Shilole amefunguka na kusema ya kuwa yeye kwa sasa amejikita kuwekeza katika vitu vingine ikiwemo ardhi na siyo magari kama wengine ambavyo wanafanya.

 

SOMA PIA:Rosa Ree Aja Na Ngoma Ya I’m Not Okay

 

Mwanamama huyo Shilole ambaye pia ni mmiliki wa migahawa maarufu ya Shishi Food aliyasema hayo wakati alipokuwa akitambulishwa kama balozi wa Homebase kampuni inayojishughulisha na usambazaji wa vifaa vya majumbani haswa vifaa vya jikoni.

 

 

 

Shilole pia alieleza ya kuwa yeye ni mama anawatoto tofauti na wengine ambao wananunua ma Range Rover huku pia akieleza ya kuwa yeye kwa upande wake amenunua nyumba ambazo kwake ni kama mtaji ambazo anazitumia kama nyumba za kupangishia wapangaji.

 

Hali Kadhalika pia mshiriki huyo wa tuzo za TMA amesema ya kuwa kwa upande wake yeye anastahili kabisa kuwania tuzo hizo ana kuhusiana na Babalevo kumsema hakustahili hizo ni stress kwa kuwa Babalevo hakupata hiyo nafasi

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!